Tuesday, June 12, 2012

UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2012 JIJINI MBEYA

 


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati) akiwasha mwenge wa uhuru kuashiria kuanza kwa mbio za mwenge huo kwa mwaka 2012 leo katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. Mwenge huo utakimbizwa kwenye jumla ya Halmashauri za wilaya, Manispaa na miji 157 na kuongozwa na kauli mbiu ya Sensa ya watu na Makazi ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo yetu Shiriki kuhesabiwa Agosti 26.

Waziri Mkuu  Mizengo Pinda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa vipeperushi vya elimu ya sensa ya watu na makazi itakayofanyika nchini kuanzia Agosti 26 mwaka huu wakati wa uzinduzi wa mbio za mwenge leo jijini Mbeya. Kushoto ni Kamishna wa Sensa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Hajjat Amina Fatma Mrisho.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangara (kushoto) akimtambulisha  kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kiongozi wa mbio za mwenge mwaka 2012 Kepteni Honest Erenest Mwanossa kutoka Dar es salaam (kulia).
Kiongozi wa mbio za Mwenge Mwaka 2012, Kepteni Honest Erenest  Mwanossa kutoka Dar es salaam akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda tayari kwa kuukabidhi kwa viongozi wa Mkoa wa Mbeya tayari kwa kukimbizwa kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2012, Kepteni Honest Erenest  Mwanossa (kulia) akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro tayari  kwa kukimbizwa kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa huo kabla ya kuelekea mkoani Iringa

credits; mwaikenda

No comments:

Post a Comment