Tuesday, June 19, 2012

DOLA MILIONI 148 HUVUSHWA NCHI ZA NG'AMBO KUTOKANA NA MIANYA YA RUSHWA TOKA AFRIKA.



ARUSHA
JUMLA ya  kiasi cha dola za Kimarekani Bilion 148   huwa zinapotea
ndani ya Nchi za bara la Afrika kila mwaka kutokana na kuwepo kwa
mianya mingi ya rushwa  na badala yake fedha hizo zinapelekwa katika
nchi za Ugaibuni hali ambayo inasababisha madhara makubwa sana kwa
nchi ya A frika


Hayo yameelezwa na mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana
na Rushwa (TAKUKURU)Dkt Edward hosea wakati akizungumza katika mkutano
wa bodi ya ushauri wa masuala ya Rushwa kwa nchi za bara la Afrika
jijini hapa


Aidha dkt Hosea alisema kuwa kiwango hicho cha fedha hupotea kutokana
na baadhi ya mianya ya Rushwa ambayo imo kwenye nchi hizo na badala
yake fedha hizo zinapelekwa kwenye nchi za Ugaibuni


Alifafanua kuwa kutokana na hali hiyo ya upotevu wa fedha hizo
unachangia kwa kiwango kikubwa sana hata kukithiri kwa rushwa ndani ya
Nchi hizo hali ambayo nayo inachangia hata maendeleo duni ya nchi hizo
za bara la Afrika


“hiki ni kiwango kikubwa sana cha fedha ambazo zinapotea
kusikojulikana lakini mpaka sasa tumeshaanza kuweka mikakati
mbalimbali ya kuhakikisha kuwa nchi za bara la Afrika hazikumbwi na
rushwa ingawaje pia changamoto ya kupambana nayo ni kubwa
sana”Aliongeza Dkt Hosea.


Katika hatua nyingine alisema kuwa mpaka sasa kwa Upande wa Serikali
ya Tanzania tayari imeshatoa kiwanja kwa ajili ya   kujenga ofisi ya
bodi ya kupambana na Rushwa ambapo mchakato huo pia utasaidia sana
kupunguza wimbi kubwa sana la Rushwa hapa nchini.


Dkt Hosea alisisitiza kuwa ujenzi wa jengo hilo la  kupambana na
rushwa utaaanza mara baada ya bunge  Kupitisha bajeti yake ambapo
jengo hilo litajengwa ndani ya eneo la Kisongo mkoani Arusha


“kwa sasa tunafurai sana kwa kuwa ujenzi wa jengo hili umeshawekwa
katika mikakati na kitu ambacho tunasubiri ni bajeti yake na
tunachokiamini ni kuwa kupitia bodi hii tutaweza kuendelea kudhibiti
mianya ya rushwa ndani ya Nchi za bara la Afrika”aliongeza Dkt Hosea

No comments:

Post a Comment