Tuesday, June 19, 2012

DOLA MILIONI 148 HUVUSHWA NCHI ZA NG'AMBO KUTOKANA NA MIANYA YA RUSHWA TOKA AFRIKA.



ARUSHA
JUMLA ya  kiasi cha dola za Kimarekani Bilion 148   huwa zinapotea
ndani ya Nchi za bara la Afrika kila mwaka kutokana na kuwepo kwa
mianya mingi ya rushwa  na badala yake fedha hizo zinapelekwa katika
nchi za Ugaibuni hali ambayo inasababisha madhara makubwa sana kwa
nchi ya A frika


Hayo yameelezwa na mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana
na Rushwa (TAKUKURU)Dkt Edward hosea wakati akizungumza katika mkutano
wa bodi ya ushauri wa masuala ya Rushwa kwa nchi za bara la Afrika
jijini hapa


Aidha dkt Hosea alisema kuwa kiwango hicho cha fedha hupotea kutokana
na baadhi ya mianya ya Rushwa ambayo imo kwenye nchi hizo na badala
yake fedha hizo zinapelekwa kwenye nchi za Ugaibuni


Alifafanua kuwa kutokana na hali hiyo ya upotevu wa fedha hizo
unachangia kwa kiwango kikubwa sana hata kukithiri kwa rushwa ndani ya
Nchi hizo hali ambayo nayo inachangia hata maendeleo duni ya nchi hizo
za bara la Afrika


“hiki ni kiwango kikubwa sana cha fedha ambazo zinapotea
kusikojulikana lakini mpaka sasa tumeshaanza kuweka mikakati
mbalimbali ya kuhakikisha kuwa nchi za bara la Afrika hazikumbwi na
rushwa ingawaje pia changamoto ya kupambana nayo ni kubwa
sana”Aliongeza Dkt Hosea.


Katika hatua nyingine alisema kuwa mpaka sasa kwa Upande wa Serikali
ya Tanzania tayari imeshatoa kiwanja kwa ajili ya   kujenga ofisi ya
bodi ya kupambana na Rushwa ambapo mchakato huo pia utasaidia sana
kupunguza wimbi kubwa sana la Rushwa hapa nchini.


Dkt Hosea alisisitiza kuwa ujenzi wa jengo hilo la  kupambana na
rushwa utaaanza mara baada ya bunge  Kupitisha bajeti yake ambapo
jengo hilo litajengwa ndani ya eneo la Kisongo mkoani Arusha


“kwa sasa tunafurai sana kwa kuwa ujenzi wa jengo hili umeshawekwa
katika mikakati na kitu ambacho tunasubiri ni bajeti yake na
tunachokiamini ni kuwa kupitia bodi hii tutaweza kuendelea kudhibiti
mianya ya rushwa ndani ya Nchi za bara la Afrika”aliongeza Dkt Hosea

Sunday, June 17, 2012

TAKUKURU NACHINGWEA YASHIRIKI KWENYE UELIMISHAJI UMMA WAKATI WA MBIO ZA MWENGE.

Viongozi wa ngazi ya wilaya wakishika Mwenge.


Umati ukishuhudia mwenge


Machapisho ya Takukuru yalioneshwa na kugawiwa kwa wananchi.


Uelimishaji umma ukiendelea na mtandao wa takukurunachi ulifunguliwa.

Wednesday, June 13, 2012

TAKUKURU LINDI YAFANYA MKUTANO NA MAHAKIMU WAKAZI WA WILAYA NA MKOANI LINDI.


Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Lindi Bw. Ndunguru(katikati) akiwa pamoja na Mratibu wa NACCSAP  wa Lindi Bw. Kuhanda (kushoto) na Bi. Lilian, Hakimu Mkazi Lindi wakisikiliza hoja mbalimbali za mkutano huo ulioitishwa na TAKUKURU Lindi ili kubadilishana uzoefu juu Uendeshaji kesi Mahakamani. Mkutano ulifanyika majuma mawili yaliyopita Ukumbi wa Takukuru Lindi


Wajumbe wa Mkutano huo wakimsikiliza Mh. Ndunguru akitoa mada yake juu ya Wajibu wa Mahakimu na Waendesha Mashtaka katika kutoa Haki.


Mafunzo yakiendelea.


Mahakimu Wakazi na Waendesha Mashtaka wakisikiliza.

Tuesday, June 12, 2012

UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2012 JIJINI MBEYA

 


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati) akiwasha mwenge wa uhuru kuashiria kuanza kwa mbio za mwenge huo kwa mwaka 2012 leo katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. Mwenge huo utakimbizwa kwenye jumla ya Halmashauri za wilaya, Manispaa na miji 157 na kuongozwa na kauli mbiu ya Sensa ya watu na Makazi ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo yetu Shiriki kuhesabiwa Agosti 26.

Waziri Mkuu  Mizengo Pinda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa vipeperushi vya elimu ya sensa ya watu na makazi itakayofanyika nchini kuanzia Agosti 26 mwaka huu wakati wa uzinduzi wa mbio za mwenge leo jijini Mbeya. Kushoto ni Kamishna wa Sensa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Hajjat Amina Fatma Mrisho.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangara (kushoto) akimtambulisha  kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kiongozi wa mbio za mwenge mwaka 2012 Kepteni Honest Erenest Mwanossa kutoka Dar es salaam (kulia).
Kiongozi wa mbio za Mwenge Mwaka 2012, Kepteni Honest Erenest  Mwanossa kutoka Dar es salaam akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda tayari kwa kuukabidhi kwa viongozi wa Mkoa wa Mbeya tayari kwa kukimbizwa kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2012, Kepteni Honest Erenest  Mwanossa (kulia) akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro tayari  kwa kukimbizwa kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa huo kabla ya kuelekea mkoani Iringa

credits; mwaikenda